WINGU LA HABARI.
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda leo amekutana na wawekezaji kutoka China kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuangalia namna ya kufanya uwekezaji kwa kujenga viwanda hapa nchini.
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Makonda amesema kuwa kutokana na malengo yaliyo wekwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa kila mkoa unapaswa kuwa viwanda 100.
Amesema kuwa wawekezaji hao watakwenda kuwekeza mkoa wa Tanga pamoja kunduchi jijini Dar es Salaam ambapo watawekeza miradi yenye thamani ya Dola bilioni 3.
"Kazi ya serikali ni kuweka mazingira ya uwekezaji na hawa ndugu zetu nilizungumza nao nilipotembelea huko kwao mwaka wa jana" amesema Makonda.
Hata hivyo amefafanua kuwa mkoa wa Dar es Salaam wilaya ya Kigamboni kutegwa kiwanda kikubwa zaidi barani afrika chenye ukubwa mita za mraba milioni tano (Square meter).
"Kuna mwekezaji mwingine ameonyesha nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari,nawaomba wafanyabiashara pamoja na vijana wetu mchangamkie fursa za kibiashara pamoja na ajira" amesema Makonda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jimbo la Gwangzou , Xie zhenghy kutoka China amesema kuwa wao wapo tayari kwa uwekezaji na katika nchi ambazo zitaendana kiutamaduni kama ilivyo Tanzania.
Amesema kuwa china imekuwa na nafasi kubwa ya kuwekeza barani Afrika ambapo imekuwa na uwekezaji mkubwa nchini Misri.
Ameeleza kuwa uwekezaji watakaofanya hapa nchini ni ule unaendana na kauli mbiu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment