WINGU LA HABARI
Afisa Masoko
Mwandamizi wa DSE, Marry Kinabo
Soko La Hisa La Dar Es Salaam 2017
Mtaji mkubwa wa soko umeongezeka kwa asilimia 10.11% kwa
mwaka 2017 tukilinganisha na mwaka 2016, na mtaji wa soko wa makampuni ya ndani
nao pia umeongezeka kwa asilimia 31.05% kwa mwaka 2017.
Ndani ya Mwaka 2017 pia kulikuwa na mauzo ya awali ya hisa
za Vodacom Tanzania Plc ambayo yamechangia ongezeko la waekezaji 40,000 na pia
kukuza mtaji wa soko kwa takribani trilioni 2.
Mauzo ya Hisa 2017
Mauzo ya hisa kwa mwaka 2017 yameongezeka kutoka Shilingi bilioni
420 ya mwaka 2016 hadi Shilingi bilioni 510 ya mwaka 2017.
Vile vile na idadi ya hisa zilizo uzika na kununiliwa sokoni
pia imeongezeka kutoka hisa milioni 194 mwaka 2016 hadi hisa milioni 257 kwa
mwaka wa 2017.
Hati fungani 2017
Mwaka 2017 hatifungani zenye thamani ya Shilingi bilioni
748.7 ziliuzwa kwa gharama ya shilingi bilioni 653, hili ni ongezeko kubwa sana
tukilinganisha na mwaka 2016 ambapo hati fungani zenye thamani ya shilingi
bilioni 556.7 ambazo ziliuzwa kwa gharama ya shiliningi bilioni 428.
No comments:
Post a Comment