Baadhi ya wafanyabiahara wa Soko la Mabibo wakimsikiliza MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda
WINGU LA HABARI
Kufuatia amri ya mahakama ya kuwataka wafanyabiashara wa soko la soko la Ndizi Mabibo lililopo Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwataka kuondoka eneo hilo ambalo ni mali ya kiwanda cha nguo urafiki mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda amekamatwa amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na Kampuni ya Udall ya Yono auction mart na kukubali Amana kuwaongeza muda wa miezi minne ili wajiandae kuondoka huku wakitafuta eneo la kwenda kufanya biashara.
Mhe. Makonda ameyasema hayo leo alipotembelea soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara hao , ambapo amesema anataka watu wafanye biashara eneo la kudumu na siyo la kuhamahama kama inavyotokea sasa.
"Wafanyabiashara wote mlioko hapa mtafanya biashara kwenye hili eneo kwa muda wa miezi minne hamtaondolewa leo wala kesho kama ilivyokuwa inatakiwa ifanyike kwa hiyo nimeongeza siku 120 nimemuelekeza mkuu wa wilaya ya Ubungo tayari kuna eneo limekwisha patikana tunatakatukamilishe utaratibu wa uhalali wa lile eneo ili watu wakiend pale wasipate matatizo kama haya ynayojitokeza ya kufukuzanafukuzana "Amesema Mkonda
Amesema soko la ndizi litakalohamishwa kwenda eneo liliopatikana litakuwa ni soko la kimataifa litakalotambulisha wilaya ya Ubungo kuwa na soko la kisasa na lenye ubora kwa Mkoa wa Dara es Salaam, na kila anaefanya biashara katika soko la mabibo ndio atakayekuwa anafanya biashara katika eneo lililopatikana.
" haitafanyika kama maeno mengine yakwamba uanapewa eneo alafu linakuja kuwa la watu wengine hautatoka kwenye hilo soko hautafukuzwa kama ambavyo ilikuwa inatikiwa kufanyika hapa, Mtatoka wote kwa pamoja kwa umoja wenu kwenda kwenye hilo eneo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zenu za biashara”amesema.
Aidha Makonda amesema hukumu ya mahakama iliwataka waondoke katika soko hilo siku ya jumamosi iliyopita lakini Serikali ya awamu ya tano imeweza kufanya amazungumzo na kampuni ya YONO na kuweza kukubali kutoa muda huo ili wafanyabiashara hao kuendelea kujipatia kipato kwa shughuli zao za biashara.
Pia amesema eneo la soko lililopatikana litakuwa tofauti na hilo la mabibo kwani litakuwa na miundo mbinu bora, ili kuweza kuruhusu wateja wa aina mbalimbali kufika kufanya manunuzi katika soko lenye ubora na viwango bora zaidi.
No comments:
Post a Comment