WINGU LA HABARI.
Kocha mkuu wa timu ya Majimaji ya Mkoani Ruvuma, Peter Mhina amesema anajipanga kuhakikisha kikosi chake kinalipiza kisasi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) inayoratajiwa kuchezwa Januari 31 au Februari Mosi mwaka huu.
Kikosi cha Majimaji
Majimaji inayoendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Majimaji Songea chini ya kocha huyo, ilichapwa na Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mchezo wao wa 11 wa Ligi Kuu Tanzania Bara ,hali ambayo kocha Mhina amesema anajipanga kulipa kisasi.
Taarifa iliyotolewa na Kocha huyo kupitia kwa Afisa Habari wa klabu hiyo, Onesmo Ndunguru ilisema kwamba timu inajiandaa vyema kuhakikisha inawachapa Ruvu Shooting na kusonga mbele katika michuano hiyo.
Mhina alisema ingawa ameipokea timu hiyo hivi karibuni lakini rekodi zinaonyesha kuwa Majimaji haijawahi kufika roundi ya tatu ya michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake .
Alisema "Nataka niwaaminishe wanasongea kwamba nipo hapa kwa kusudi la kuipaisha Majimaji kwenye FA lakini kwenye Ligi Kuu kuhakikisha tunamaliza ligi katika nafasi nzuri zaidi kimsimamo’.
‘’Niliwasoma wachezaji wake tulipokutana nao kwenye mechi ya Ligi Kuu ,mbinu na mfumo wao ninao kwa hiyo hainipi shida jinsi ya kuwakabili hawa Ruvu Shooting,’’alisema Mhina.
Alisema maandalizi wanayofanya ni kwa ajili ya mapambano ya Ligi kuu ambapo mechi mbili zilizo mbele yao ni kama fainali kutokana na ubora pamoja na nafasi waliopo wapinzani wao.
Mhina alisema "Januari 18 tuna mechi na Azam FC na baada ya hapo tutawasubiri Singida United tarehe 22 mwaka huu ambapo nao ukiangalia si mchezo rahisi kutokana na walivyokuja wa moto pamoja na kwamba ni wageni Ligi Kuu."

No comments:
Post a Comment