Mshindi wa shindano la kutunisha misuli Erick Majura akiwa upande wa kulia akishika kombe baada ya kushinda.
WINGU LA HABARI
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM,
Mshindi wa shindano la kutunisha misuli Erick Majura amsema mara baada ya kutwaaushindi katika ukumbi wa Mayfair jijini Dar es Salaam Desemba mwaka jana bado anaendelea kujiweka fiti kuelekea shindano jingine litakalo fanyika nchini Nigeria.
Hali hiyo inakuja baada ya mwishoni mwa mwaka jana ambapo shirikisho la Ujenzi waMwili Tanzania (TBBF) kwa kushirikiana na Kampuni waandaaji wa shindano hilo Pilipili intertainment kuandaa vema shindano hilo.
Majura alisema baada ya kuwa mshindi na kuweza kutwaa gali na kitita cha sh.Milion 10,000 kwa kuwagalagaza vibaya wenzake walioshiriki , taswira yake kwa sasa inawazia kuendelea mbele zaidi ambapo anajiandaa kwenda kushiriki shindano kubwa la Afrika katika mchezo huo
wa misuli.
"Najua tutakwenda kuchuana na wenzangu wenye sifa kama mimi , tayari naendelea kujipanga kwa kufanya mazoezi vema katika mazoezi yangu ya kila siku kwa mwenyezi Mungu ni mkubwa na shukuru sana kwa kuwa mshindi kwa mwaka jana hatua inayoniwezesha kutinga katika shindano la Afrika mwishoni mwa mwaka huu,"alisema Majura.
Wakati huo huo mmiliki wa Gym iliyomwandaa mpaka kufikia kutwaa ushindi kwa mshindi huo Mohamed Ali ,ambaye pia ni mmiliki waGym ya mazoezi ya Gymkhana Dar es Salaam amesifia mchezo huu, na kusema kua shindano hilo mwaka jana liliofanyika katika ukumbi wa Mayfai jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwakajana kuwa lilifanyika vema na kuwa limeongeza
hali ya ushawishi kwa wanamichezo.
Ali alimpongeza mshindi huyo aliyeibuka na kitita cha Shilingi Milioni 10 na kusema ni moja ya mafanikio ya kuutangaza mchezo huo kwa siku za hivi sasa .
Alisema mchezo huo umekuwa ukifanyika nchini kuanzia miaka ya 1990
na kuwa safari katika maisha ya mchezo huo unaonekana kufikia malengo
mengine hivyo onesho hilo limeweza kuonesha hamasa mpya kwa jamii .
"Napenda kuona Wadau katika mchezo huu, kuendelea kushiriki vema kwani hamasa mpya kama hii walionesha waandaaji kwa kuandaa shindano katika uwezo mkubwa, ni ushawishi mpya kwa vijana wapya,"alisema Ali.
Ali alisema zawadi zilizoandaliwa kwa washindi na maandali ya mchezo
huo kweli waandaaji walijitaidi kufanya maandalizi mazuri .
Mdau huyo mkubwa katika mchezo huo ambaye mwaka 2014 aliandaa shindano lake lililoitwa ( The Most Musicular Man Tanzania 2014) na kufanikiwa kuendela kuonesha taswira ya watu kuendelea kuwa na hamasa juu ya kushiriki katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment