Na Noel Rukanuga.
Amemwomba waziri, kutenga asilimia 10 ya bajeti ya serikali kuwekeza kwenye kilimo ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya kilimo.
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage amezitaka Mamlaka husika katika Serikali kuwapa watu elimu ili kujua viwango vya bidhaa wanazopaswa kuzalisha hapa nchini na si kuwakamata kwa kutojua viwango.
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua warsha ya wadau wa kilimo leo jijini Dar es Salaam.
Mwijage ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua warsha ya kitaifa siku mbili ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT).
"Ili twende vizuri na kufanikiwa katika sekta ya viwanda. Mamlaka zote za serikali zisifanye kazi ya upolisi zifanye kazi ya ualimu na lisema na nipo tayari kuhukumiwa, "amesema.
"Mtu anafanya 'packaging' anatengeneza bidhaa yake mnamwambia amekosea umweleze maana yake ni nini.... Muwafundishe hao watu ambao mimi napoteza muda kuwahamasisha kujenga viwanda, "amesema na kuongeza. "Mimi siwezi kushawishi halafu mwenzangu anafungia. Kwa sasa mazingira ya biashara ni mazuri."
Amesema serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya kufanya biashara na kuwa mtu anayetaka kuweka kiwanda aanze halafu mamlaka ya mazingira na mamlaka ya viwango (TBS) wafuate.
"Tunajenga viwanda ili tutengeneze soko la mazao yenu, viwanda ni masoko tunajenga viwanda kwasababu asilimia 65 ya watanzania ni vijana na wengi Hawana kazi, "amesema.
Waziri Mwijage amesema ujenzi wa viwanda si kuzalisha bidhaa pekee bali ni pamoja na kutengeneza ajira.
Awali, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa ACT, Dk. Sinare Sinare amemshukuru rais kwa kuwaondolea tozo katika mazao.
Amesema wanaamini kichocheo cha uzalishaji ni soko na changamoto iliyopo ni soko kwa nchi za Afrika Mashariki.
"Afrika Mashariki hakuna mchele unaopendwa kama unaotoka Tanzania, lakini fursa hiyo inashindwa kutumika ipasavyo kutokana na mwingiliano wa masoko, "amesema.
No comments:
Post a Comment