MKURUGENZI WA WIRAYA YA NKASI MKOANI RUKWA ASIMAMISHWA KAZI - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, December 8, 2017

MKURUGENZI WA WIRAYA YA NKASI MKOANI RUKWA ASIMAMISHWA KAZI

Waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi mkurugenzi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na  matumizi mabaya yaliyoisababishia serikali hasara ya bilioni  7

Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo

Leo mjini Dodoma Jafo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

"Natumia sheria ya serikali za mitaa sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," amesema Jafo

Amesema fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa kijiji cha Kamwanda ambako mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.

Hivyo amemuomba waziri wa maji na umwagiliaji, Isaak Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika kijiji cha Kamwanda wilayani humo.

Katika mkutano wa nane wa bunge, mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Keissy alilalamika bungeni akimtaka rais akamkabidhi watumishi wake kwani ni wabadhirifu.

Keissy alisema miradi ya maji ndiyo inaonekana kuhujumiwa zaidi ikiwemo kununua vitu bandia na kufanya udanganyifu kwenye manunuzi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here