Baada ya kupata ufaulu mzuri na kuongoza kitaifa katika matokeo ya Darasa la saba mkoa wa Dar es Salaam,leo umetangangaza kuwa hakutakuwepo na wanafunzi wa chaguo la pili badala yake wanafunzi wote wamepangiwa shule moja kwa moja.
Akizungumza katika Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2017 wa mkoa huo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando amesema kuwa katika matokeo ya Darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 58,573 walifanya sawa na asilimia 100% wote wamepangiwa shule na Wataanza kidato cha kwanza January 2018.
Amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za ufaulu mzuri zaidi ni 68, wavulana 35 na wasichana 33.
Wanafunzi walio walio chaguzi wa shule za ufundi ni 74,wavulana 68na wasichana 6,shule za bweni kawaida no 24wavulana 12 na wasichana 12.
Aidha amesema, wanafunzi 1,931wamechaguliwa kujiunga na shule za mkoa zinazo chukua wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wavulana ni 850 na wasichana 1, 081.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule za serikali za wananchi ni 56,299 ikiwemo wavulana 27,035 na wasichana 29,264 huku wanafunzi wenye uhitaji maalum waliopangiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ni 101wavulana wakiwa ni 58na wasichana 43.
Amefafanua kuwa, waliochaguliwa Manispaa ya Ilala ni wanafunzi 19,236,kigamboni 2,803,Kinondon 10,885 Temeke15, 323na Ubungo ni 10,326.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo Jumla ya nafasi 4,685 katika shule za pembenizomwajiji zimebaki wazi kwa sababu ya umbali uliopo kati ya shule ya msingi waliposoma wanafunzi na mahali shule zilipo, nafasi zizo baki kwa Manispaa ya Ilala ya Ilala (mjini) ni 887,kigamboni590, Kinondon 1,718 na Ubungo 1,490.
Akizungumzia asilimia, amesema wanafunzi waliojiunga na shule za secondari kwa waliofanya mtihani kwa mkoa ni asilimia 87.82%. katika Manispaa ya Ilala (mjini) ni asilimia 92.48.Ilala (Vijijini) asilimia 84.42.Manispaa ya Kinondoni 93.02%Temeke 81.74%.Kigamboni 91.10% na Ubungo ni 89.01.
Pamoja na hayo Mbando amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuwa peleka watoto wao shuleni waliopangiwa tarehe 8 January 2018bila kukosa, na kuwakumbusha wakuu wa shule 147 zinazo pokea wanafunzi kuzingatia waraka no 2 wa 2016 unao husu uendeshaji wa elimu bure bila malipo.
No comments:
Post a Comment