Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu )
Mhe.Jenista Mhagama ameielekeza Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji
wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), kuongeza Thamani Biashara za
Mifugo wilayani Longido kwa kutatua kero zote za wafanyabiashara wa
mifugo wilayani humo.
Mhagama
ametoa maagizo hayo baada ya kukagua Soko la kimkakati lililojengwa na
Serikali kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Programu ya Miundo mbinu
ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF). Soko
hilo litawanufaisha wananchi wapatao 14,2000 wa wilayani Longido ambapo asilimia
95 ni wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za mifugo.
Soko
hilo la kimkakati ambalo halijafunguliwa rasmi , tayari halmashauri ya wilaya
hiyo imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106 kwa mwaka
2016/2017 ambapo kwa makusanyo hayo yamewezesha halmashauri hiyo kuvunja rekodi
ya miaka kumi iliyopita kwa kukusanya shilingi bilioni 1.3.
Makusanyo
hayo imekuwa mara ya kwanza kwani awali mapato yake yalikuwa chini ya
bilioni moja. Aidha umuhimu wa soko hiloumejidhihirisha pale Halmashauri
ilivyoweza mwezi Novemba kutoa asilimia 10ya mapato yake kwa wananwake na
Vijana ikiwa nikwa asilimia5 kwakilakundi na hii ikiwa nimara ya kwanza kwa
Halmashauri hiyo kuweza kutekeleza hilotangu kuanzishwa kwake.
MIVARF; ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha
Vijijini iliyobuniwa na serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki
ya Maendeleo ya Afrika (ADB). Programu hii inatekelezwa
katika mikoa 29 ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani tangu mwaka 2011
No comments:
Post a Comment