JACOB ZUMA ASEMA MUSTAKABALIWA WA ANC UPO KATIKA TISHIO - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, December 16, 2017

JACOB ZUMA ASEMA MUSTAKABALIWA WA ANC UPO KATIKA TISHIO

Zuma anajiuzulu kama mwenyekiti wa ANC baada ya kuhudumu kwa muongo mmoja





Haki miliki ya pic

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio.
Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho.
Rais Zuma amezungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka.
Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura.
Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa.
Wagombea wakuu wanaopigiwa upatu kumrithi kama kiongozi wa chama hicho ni naibu rais, Cyril Ramaphosa, na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Nkosazana Dlamini-Zuma, mkewe Zuma wa zamani.
Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa.
Chama hicho tawala kimekuwa kikipoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na tofuati za ndani ya chama chenyewe.
Lakini bado kina umaarufu katika ulingo wa kisiasa baad ya kuwepo madrakani kwa miaka 23.
Kikao hicho kinakutanaisha wajumbe takriban elfu tano mjini Johannesburg.
Wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.

Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril RamaphosaHaki miliki ya pichaREUTERS/AFP
Image captionWagombea wakuu ni Nkosazana Dlamini-Zuma na Cyril Ramaphosa

Kivumbi hasa kipo katika Kinyanganyiro cha kumrithi rais Zuma, kama kiongozi wa chama- ni kati ya mkewe wa zamani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma -- ambae pia aliwahi kuwa waziri na vilevile alikuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika.
Lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanaomuunga mkono makamu wa sasa Cyril Ramaphosa,
Mvutano huu pamoja na kashfa chungu nzima hasa za rushwa zinazomuandama rais Jacob Zuma zimeongoza hofu za kugawanyika kwa ANC. Chanzo BBC.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here