Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles
Mwijage akizungumza na waandishi wa habari jijini leo Dar es Salaam.
Na Noel
Rukanuga.
Wizara ya
Viwanda na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleoa ya Biashara Tanzania (Tan
Trade) imewataka wamiliki wa viwanda vidogo, kati na vikubwa kushirikia katika
maonyesho ya pili ya bidhaa za viwanda yanayotarajia kufanyika Desemba 7 hadi 11
mwaka huu.
Maonyesho hayo
yatafanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara wa mwalimu J.K Nyerere
(sabasaba) vilivyopo barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, amesema kuwa zaidi ya viwanda 500 wanatarajia kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu.
Amesema kuwa kwa mwaka huu idadi ya washirikiki inatarajiwa
kuongezeka kutokana katika kipindi cha miaka miwili kuna viwanda vipya 3,306 ambavyo
vinauwezo wa kuajili zaidi ya watu 10.
Mhe. Mwijage amefafanua kuwa katika monyesho ya mwaka wa jana
kulikuwa na makampuni 472 pekee ambayo yalishiriki.
“Lengo la maonesho ni kuwaweka wadau wa viwanda pamoja ili wapata
fursa ya kujadiliana, kubadilisha uzoefu wa kuzalisha bidhaa pamoja kuuza nje
ya nchi,”amesema Mwijage.
Amesema kuwa maonesho hayo mwaka huu yanabeba kauli mbiu isemayo “Tanzania sasa tunajenga viwanda” ikilenga kuwaaminisha wananchi juu ya falsafa na dhima ya ujenzi wa viwanda wa uchumi wa viwanda.
Amesema kuwa meonesho hayo yatawakutanisha wadau wa viwanda
ikiwemo wazalishaji wa malighafi, taasisi zinazotoa huduma mbalimbali kwa wenye
viwanda na taasisi zinazowezesha wenye bidhaa kutoka kiwandani mpaka kufikia
kwa mtumiaji.
Amesema wakati wa maonesho desemba 11, 2017 itakuwa siku maalumu ya viwada Afrika ambayo itaratibiwa na kwa ushirikiano na Taasisi za Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO).
Mhe. Mwijage amesema wizara yake kupitia Mamlka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) imewakaribisha watanzania wanaomiliki viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kushiriki maonesho hayo.
Katika hatua nyengine amewataka wafanyabiashara
kuanza wakiwa na mitaji midogo ili waweze kuendelea na kuapata fursa ya kukuza
uchumi kupitia viwanda.

No comments:
Post a Comment