WAWILI WAFARIKI KATIKA MLIPUKO CHINA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, November 26, 2017

WAWILI WAFARIKI KATIKA MLIPUKO CHINA

Mlipuko huo umesbaabisha uharibifu wa mali ikiwemo nyumba na magariHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMlipuko huo umesbaabisha uharibifu wa mali ikiwemo nyumba na magari
Maafisa nchini China wanasema watu wawili wamefariki na 30 wakajeruhiwa katika mlipuko kwenye kiwanda kimoja mjini Ningbo, kusini mwa Shanghai.
Mlipuko huo umesababisha vifo vya wawili na wengine wengi wakajeruhiwa.
Madirisha ya majengo yaliyo umbali wa hadi kilomita moja kutoka eneo la mlipuko yamepasuka.
Inakisiwa kuwa mitungi ya gesi imesababisha mlipuko huo, japo polisi wanaendelea na uchunguzi.
Picha zilizotolewa zinaonyesha wafanyikazi wa mjego wakiondoa watu kutoka kwenye eneo la mlipuko ambapo majengo yameharibiwa na magari yamebondwa.
Ambulensi zimeonekana zikiondoa watu kutoka kwenye eneo la mlipuko hadi kwenye hospitali zilizo karibu.
Mji wa Ningbo unajulikana kwa viwanda vya kutengeneza magari. Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here