Wahitimu wa mafunzo ya mgambo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kutumia mafunzo waliyoyapata, kwa kufanya shughuli za kizalendo na kuepuka kuwa chanzo cha uhalifu na maovu katika jamii.
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva alipokuwa akifunga mafunzo ya Mgambo kundi la 55 lenye jumla ya washiriki 815 waliohitimu leo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuwa wazalendo na kufanya shughuli mbalimbali za ulinzi shirikishi katika jamii.
"Mafunzo mliyopata myatumie kwa kufanya shughuli mbalimbali za kizalendo kwa kuokoa maafa,Msiende kuwa chanzo cha Maovu na uhalifu huko mitaani wekeni Uzalendo mbele" Amesema Mh. Ganiva
Aidha amewapongeza washiriki wote waliohitimu mafunzo hayo ambapo amewataka washauri wa kila wilaya waweze kuwapatia barua watakayopeleka kwa mtendaji wa kila kata ili waweze kuwekwa kwenye Ulinzi shirikishi katika katika kila mtaa.
Hata hivyo Lyaniva ameyataka makampuni binafsi ya ulinzi kuchukua walinzi kwa kufuata taratibu na sheria ikiwa ni pamoja nakuweka wazi mkataba wamalipo ya mishahara yao na kuwataka kuacha kuajiri mgambo kinyemela badala yake waombekupitia kwa mshauri wa mgambo Wilaya.
Katika hafla hiyo Mh Fellix Lyaniva , amekagua gwaride la Mgambo hao, pamoja na kutoa vyeti kwa washiriki wa kila Wilayairiki kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, ambazo ni Ilala, Temeke, Kigamboni Ubungo na Kinondoni.
washiriki waliohitimu mafunzo hayo wameonyesha maonyesho mbalimbali waliyoyapa kipindi chote cha mafunzo muda wa miezi minne ambapo wameonyesha, onyesho la mapigo ya kareti, Gwaride kupita mbele kwa mwendo wa pole na haraka Onyesho la kwata ya kimyakimya, pamoja na onyesho la Singe.
Kwa upande wake mshauri wa Jeshi la Akiba mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Ismail amemshukuru Mh mgeni rasmi kwa kufika kufunga mafunzo hayo ambapo ameiomba serikali kuangalia changamoto za gharama ya mafunzo ambapo washiriki wanaopenda kujiunga naafunzo wanashindwa kumudu gharama hiizo.
No comments:
Post a Comment