Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports nchini Rwanda Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kataut beki wa zamani wa Rayon Sports na mume wa muigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya na kufanikiwa kupata mtoto mmoja amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.
Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza Kataut alikuwa mazoezini jana asubuhi, kabla ya kifo chake mara ya mwisho aliichezea Stand United ya Shinyanga wakati akitokea Cyprus.
Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment