Kiwango cha kutoa na kupokea rushwa kimepungua kwa asilimia 85
mpaka ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo mwaka mwaka 2014 viwango
vya rushwa ilikuwa asilimia 78.
Akitoa ripoti ya utafiti leo Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, amesema kuwa wananchi
wamebainisha kuwa uzoefu wa kuomba rushwa umepungua katika sekta zote kwa mwaka
huu ulinganisha na mwaka 2014.
Ripoti hiyo ya utafiti imeeleza kuwa katika sekta ya jeshi
la polisi rushwa imepungua kutoka asilimia 68 kwa mwaka 2014 na kufikia asilimia
39 kwa mwaka huu.
Sekta ya ardhi ni asilimia 32 hadi kufikia asilimia 18, Afya
asilimia 19 hadi asilimia 11, Maji asilimia 20 hadi asilimia 6, Mamlaka ya
Mapata (TRA) ni asilimia 25 hadi asilimia 5, NGOs ni asilimia 13 hadi kufikia
asilimia 6 kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa utafiti huo sekta ya polisi pamoja na mahakama
kwa mwaka huu ndio zinaongoza kwa kuomba rushwa kwa wananchi huku Jeshi la
polisi likiongoza ikiwa na asilimia 39 ikifatiwa na mahakama kwa asilimia 36.
No comments:
Post a Comment