MUSTAKBAL WA ZIMBABWE BAADA YA MUGABE KUJIUZULU - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 22, 2017

MUSTAKBAL WA ZIMBABWE BAADA YA MUGABE KUJIUZULU

Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani

Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa raius wa Zimbabwe pekee.
Phelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajuliakana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.
Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.
Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.
Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri. Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.
Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .
Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi. chanzo BBC
Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani
BBC
Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here