Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka taasisi ya Foundation for Civil Society kuendelea kuzijengea uwezo taasisi mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya miaka 15 ya taasisi hiyo ambapo amewataka viongozi kuendelea kuwajengea uwezo vijana ili taifa liweze kuwa na maendeleo na kufanikiwa katika uchumi.
Katika maadhimisho hayo Mhe. Mhagama alikuwa mgeni rasmi ambapo alikuwa anamwakilisha Makamu wa Rais. Samia Hassani Suluhu.
No comments:
Post a Comment