MAKAMPUNI NA MIFUKO YA BIMA YA AFYA YATAKIWA KUTOA HUDUMA YA VIUNGO BANDIA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, November 17, 2017

MAKAMPUNI NA MIFUKO YA BIMA YA AFYA YATAKIWA KUTOA HUDUMA YA VIUNGO BANDIA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akipokea Mchango wa shilingi Milion 10,  kwa ajili ya walemavu wa miguu leo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Spectrum Design Consulting Architects  Arch Jimmy  Mkenda (katikati) akizungumza baada ya kukabidhi mchango wake kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda 


Baadhi ya walemavu wakifanya mazoezi baada ya kuwekewa mguu bandia katika hospitali ya CCBRT. 
Na. John Luhende 
Mkuu wa mkoa wa Dar es  salaam Paul Makonda ameyataka Mkampuni na Mifuko ya Bima ya Afya kujumuisha gharama za matibabu ya bima zao  huduma ya kuwahudumia kununua viungo bandia watu walio katwa viuogo vya kwa ajali ama kwa kuugua ili kuwa ondolea usumbufu wanaopata kwakuwa viungo hiyo huuzwa bei ghali. 

Makonda ameyaesema hayoleo alipotembela Hospipal ya CCBRT Msasani Jijini Dr es salaamu  ambapo wanatengeneza  viungo bandia na kuwahudumia watu walio katwa  viungo  ambapo CCBRT  ilijitolea kuwahumia bure walemavu  35 walijitokeza katika kampaini iliyo alioianzisha mwezi Agost mwaka huu. 

Amesema uhitaji wa miguu bandia ni mkubwa kwani watu wamekwatwa miguu kutokana an ajali au ugonjwa wa kisukari,hivyo serikali pamoja na wadau mbalimbali tunaomba wananchi waweze kujitokeza kuchangia ili kurudisha furaha na amani kwa walemavu ili kurudi katika maisha yao kama mwanzo na kuendelea na kazi zao walizokuwa wakifanya

"Natamani kwenye msimu huu wa kwenda kufunga mwaka we we uliye salama kumrudishia furaha na amani kwa kuchangia MTU mmoja na kuleta matumaini kwa watu wa Mkoa huu wa Dar es Salaam wenye uhitaji huu wa miguu bandia" Amesema

Ameishukuru Hospital ya CCBRT kwa kuunga mkono kampeni hiyo pamoja E FM RADIO na TV E walioojitolea kuhamasisha jamii kuchangia Miguu Bandia.

"Account namba ya kuweza kuchangia yenye jina "Uchangiaji wa Miguu bandia Dar es Salaam" Namba 0150299713500 wananchi wote wanaweza kuweka hela  kokote kule na niendelee kuomba tena ni ihari yako kuweza kuwarejeshea matumaini wenzetu walipata ulemavu wa miguu kwa ajali au kutokana na ugonjwa wa kisukari". Amesema Makonda

Vilevile  amesema kuwa atazungumza na Taasisi zinazotoa Bima ya Afya ili waongeze kipengele cha Matibabu na kutoa Miguu bandia kwa watu waliopoteza Miguu kwa Ajali au Ugonjwa.

Kwa upande wake Afisa mwendishaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT  Brenda Msangi amesema wao walishirikiana na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwasaidia walemavu wa miguu na wamechangia kampeni hiyo kwa kuwasaidia watu 35  na tayari wamepataiwa miguu walemavu 21 ambapo amewataka wadau mbalimbali pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia kwani uhitaji bado ni mkubwa.

Katika hatua nyingine Makonda amepokea kiasi cha Shillingi Million 10,000,000 kutoka kampuni ya Ujenzi ya SPECTUM DESIGN ambapo Mkurugenzi wake Arch.JIMMY MKENDA amesema lengo la kutoa mchango huo waliwiwa na  kuamua kujumuika kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia waliokata tamaa baada ya kupoteza miguu waweze kurejesha furaha na amani kwa hawa waliopata ulemavu kutokana na ajali au ugonjwa wa kisukari.

Gharama za mguu mmoja wa bandia kwanzia matengenezo hadi kukamilika unagharimu shilingi milioni 1.5 kwa waliopata ajali na kukatwa miguu na waliokatwa miguu kwa Ugonjwa wa kisukari gharama yake ni milioni 4.5 hadi milioni 4.7  kwanzia unapotengenezwa hadi kukamilika na mtu kupatiwa mguu huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here