Zaidi ya Wahitimu 500 wa Chuo Cha Kodi (ITA) wametakiwa
kutumia vema elimu waliopata chuoni hapo katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kulipa
kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika Mahafali ya Kumi ya Chuo
Cha kodi (ITA) Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Yamungu Kayandabila, amesema kuwa ni vema wanafunzi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii
kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Dkt. Kayandabila ambaye ni mgeni rasmi katika Mahafali hayo ambapo
alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mapango, amesema “Serikali
itaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi katika chuo cha kodi kwa kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ili taifa
liwe na maendeleo”.
Hata hivyo amewataka wahitimu hao kuendelea na masomo
katika ngazi nyengine ili kuongeza mahalifu katika masula ya kodi jambo ambalo
linaweza kuleta chachu ya maendelo katika jamii.
Katika hatua nyengine amebainisha kuwa serikali
itaendelea kushirikiana na chuo kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili
kuhakikisha chuo hicho kinapiga hatua na kuwa msaada kwa kuzalisha wanafunzi wenye
vigezo.
“Chuo kina nafasi kubwa ya kuendelea na udahili wanafunzi wengi kwa maendeleo ya taifa”
amesema Dkt Kayandabila.
Mkuu wa Chuo Cha Kodi (ITA)
Profesa Isaya Jairo, amewataka wahitimu kwenda kuwa mabalozi kwa kukitangaza chuo
vizuri kupitia taaluma zao.
Amesema kuwa kufanya hivyo
itasaidia kuleta maendeleo kwa watanzania kuwa na mwamko wa kulipa kodi.
Hata hivyo Prof Jairo ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili chuoni ni pamoja na baadhi
ya wanafunzi wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa fedha na
kusababisha kushindwa kumudu gharama za chuo.
“Baadhi ya wanafunzi wameshindwa
kumaliza chuo kutokana na kukosa ada, hivyo tunaiomba serikali kutoa mikopo
idadi kubwaya wanafunzi wetu” amesema prof Jairo.
Prof Jairo amewataka wahitimu hao
kwenda kutatua changamoto ambazo wanakwenda kukutanz nazo ikiwemo ukosefu wa
ajira.
Amesema kuwa wahitimu hao
hawapaswi kukaa nyumbani ila wanapaswa
kutumia elimu yao kutengeneza fursa za ajira.
Aidha amefafanua kuwa chuo
kinatoa fani fupi na ndefu katika katika masula ya kodi kuanzia ngazi ya cheti
na kuendelea.
Amesema katika kuleta maendeleo
chuo hapo, Chuo kina Baraza la Uongozui ambapo kazi yao kutoa ushauri katika
masula mbalimbali ya kitaalamu chuoni hapo.
Hata hivyo ametoa zawadi mbalimbali kwa wahitimu 12 waliofanya vizuri zaidi
katika masomo ikiwa ni utaratibu ambao chuo kimejiwekea ili kutambua jitihada
nzuri ambazo zimefanywa na wanafunzi hao pamoja na kuwashajihisha wanafunzi
wanaoendelea na masomo kufanya vizuri zaidi katika masomo.
Katika fani
mbalimbali zinazotolewa katika chocha kodi jumla ya wanafunzi waliotunukiwa vyeti,
stashahada na shahada katika mahafali ni wahitimu 82 wa Cheti cha Uwakala wa
Forodha cha Afrika Mashariki yaani the ‘East African Customs and Freight
Forwarding Practising Certificate (EACFFPC).
Wahitimu 39 wa Cheti
cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Basic Technician Certificate in Customs
and Tax Management (CCTM).
Stashahada ya Usimamizi
wa Forodha na Kodi yaani (Diploma in Customs and Tax Management (DCTM)) ni wahitimu 147.
Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani
(Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM) ni wahitimu 134.
East African
Community Postgraduate Certificate in Customs Administration (PGCCA) ni wahitimu
85 na Stashahada ya Uzamili katika Kodi yaani (Postgraduate Diploma in Taxation
(PGDT) wahitimu ni 33.
Pamoja na kutunuku
vyeti stashahada, na shahada kwa wahitimu, mgeni Rasmi alitoa tuzo kwa
wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha
mwaka wa masomo wa 2016/2017 na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya
kitaaluma, ikiwa ni pamoja na jarida la Chuo cha Kodi yaani ‘Journal of the
Institute of Tax Administration’ (JITA).
Hata hivyo chuo hicho kinasherehekea miaka kumi tangu kipate ithibati (usajili)
kutoka Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Chuo cha kodi kinajivunia
miaka kumi ya mafanikio katika kutoa mafunzo ya Forodha na Kodi yanayokidhi
soko la ajira katika nyanja za forodha na Kodi ndani na nje ya nchi.
Tangu kipate usajili
wa kudumu kutoka Baraza la Vyuo vya Ufundi (NACTE), Chuo kimepanua wigo wa
taaluma kutoka kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA pekee hadi kutoa mafunzo kwa
wadau mbalimbali wa masuala ya forodha na kodi kwa nchi za Mashariki Kati na
Kusini mwa Afrika.
Kikiwa katika hatua
za mwisho za utekelezaji wa Mkakati wa tatu, Chuo cha Kodi kinaendelea na
maandalizi ya kuwa Kituo cha Umahiri wa Forodha na Kodi katika ukanda wa Afrika
Mashariki baada ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kukiteua Chuo
cha Kodi kuwa Kituo cha Umahiri Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment