
Na Mwandishi wetu.
Mahakam Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu Msanii wa
Filamu, Elizabeth Micheal (Lulu) kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada
ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven
Kanumba.
Hukumu iliyosomwa na Jaji Sam Rumanyika
imemtia hatiani Lulu kuwa alimuua msani mwenzake, Marehemu Kanumba bila
kukusudia usiku wa Aprili 7, 2012 Sinza Kinondoni Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza Lulu alifikishwa mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu , lakini baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, chini ya Jaji Rumanyika aliyesoma hukumu
hiyo leo.
Jaji Rumanyika anesema amemtia hatiani lulu kuuwa bila
kukusudia kwa kuzingatia kifungu cha 195 cha sheria.
Upande
wa Jamhuri ulileta mahakamani mashahidi wanne wakiwemo Seth Bosco ambaye ni
mdogo wake Marehemu Kanumba, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba moja na marehemu
na aliyekuwepo siku ya tukio, Dk. Paplas Kagaiga aliyekuwa Daktari wa familia
hiyo ambaye aliyefika nyumbani kwa Marehemu Kanumba mara baada ya kudondoka.
Wengine
ni Daktari kutoka kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyeufanyia uchunguzi
mwili wa Marehemu Kanumba pamoja askari ASP Ester aliyefanya upelelezi kwenye
tukio hilo pamoja na kumtia mbaroni Lulu.
Lulu
aambaye anatetewa na wakili Peter Kibatala, waliwasilisha mashahidi wa wawili
ambao ni Lulu mwenyewe aliyehadithia mazingira ya tukio na kueleza kuwa
hakuhusika kwa namna yoyote kwenye kifo cha Marehemu Kanumba.
Hata hivyo Wakili
wa Lulu, Kibatala amesema wanajipanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment