Na Noel Rukanuga.
Makandarasi nchini Tanzania wametakiwa kufanya kazi kwa umoja na ushirika, jambo ambalo linaweza kuwapa fursa katika kutekeleza majukumu ya na kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
Akizungumza leo katika hafla ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa ni fursa kwa wakandarasi kutumia mkutano huu katika kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ujenzi wa taifa.
Amebainisha kuwa ili Chama hicho kiwe na mafanikio wanapaswa kuzingatia masula muhimu katika shughuli zao za kila siku.
Miongoni mwa mamba hayo ni pamoja kufanya kazi kwa uweledi, kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, kuepuka rushwa na ufisadi, ulipaji wa kodi pamoja na kuzingatia usalama na mazingira ya kazi.
Hata hivyo Eng. Nyamhanga amesema kuwa kuna miradi mingi hapa nchini ambayo inapaswa kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa makao makuu ya serikali, mjini dodoma, ujezi wa reli pamoja na barabara.
"Ni fursa kwa wakandarasi kuweza kuchangamkia fursa hizo na serikali kazi yake kuwapa kazi wakanadarasi hapa nchini" amesema
Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandrasi Eng. Lawrence Mwakyambiki amesema kuwa lengo la mkutano ni kujadili masula mbalimbali katika utendaji wa wakandarasi ili kuleta mafanikio katika taifa.
Amesema wataweza kujitengenezea mikakati ambayo inaweza kufikia malengo ikiwemo kutoa mchango wao wa kufikia Tanzania ya viwanda.
Mwakyambiki ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao ni hapa nchini ni ukosefu wa miradi, bajeti kuwa ndogo jambo ambalo linawapa wakati mgumu.
Mkutano huo wa wakanadarasi ni Mkutano Mkuu ambao umefanyika kwa mara ya kwanza ambapo ikiwa ni sehemu ya ratiba yao ambapo utakuwa unafanyika kila mwaka Novemba 17.
![]() |
Eng. Joseph Nyamhanga |
No comments:
Post a Comment