AZAM FC YAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 29, 2017

AZAM FC YAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO

Waandishi wa habari za michezo 
Msemaji wa klabu ya Azam Fc Jaffar Idd.

Uongozi wa Klabu ya Azam umesema kuwa kwa sasa hautasajili tena mchezaji mwingine ndani ya kikosi hicho baada ya kumalizana na Mghana, Bernard Arthur na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd amesema: “Kwa sasa ndiyo tumefunga usajili kwenye kikosi chetu, hatutasajili tena mchezaji mwingine kwa sababu nafasi zimejaa, na hivi karibuni tumemuongeza mkataba kiungo wetu, Steven Kingue Mpondo raia wa Cameroon.”

Tamko hilo wamelitoa wakati dirisha dogo la usajili likiendelea kuwa hewani ambapo lilifunguliwa Novemba 15, mwaka huu na litafungwa mwezi ujao tarehe 15.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here