MHE. UMMY MWALIMU MGENI RASMI MATEMBEZI YA HISANI TAASISI YA OCEAN ROAD - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, October 27, 2017

MHE. UMMY MWALIMU MGENI RASMI MATEMBEZI YA HISANI TAASISI YA OCEAN ROAD


Mkurigenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean road Dr Julius Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari mapema leo  (hawapopichani )kuhusu matembezi yatayofanyika kesho.
Na Noel Rukanuga

Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Hospital ya Aga Khan,Hotel ya Kunduchi beach imeandaa matembezi ya hisani yanayotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu ambayo yanalengo la kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti. 

Matembezi hayo yataanzia katika taasisi ya saratani ya ocean road kunazia saa 12:30  asubuhi na kuhitimishwa saa 4:00, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe Ummy Mwalimu.


Katika kuelekea matembezi hayo takwimu za ugonjwa wa saratani ya matiti zimebainisha kuwa vifovitokanavyo na saratani hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 24ifikapo mwaka 2035 kama juhudi za kuzuia na tiba hazitaimarishwa katika nchi zote zenye uchumiwa kati.


Hata hivyo takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya duniani (WHO) zikionyesha ongezeko la wagonjwa wapya 14.1 milioni kila mwaka wanagundulika huku na wagonjwa 8.8 hufariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Saratani ya Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage amesema athari za kiuchumi
zitokanazo na ugonjwa wa saratani ni kubwa na zinaongezeka kila mwaka ambapo
mwaka 2010 zilikadiliwa kufikia dola za kimarekani trilioni 1.16.




Amesema  takwimu zinaonesha kuwa wanawake duniani kote , saratani ya matiti ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 kila mwaka wanagundulika ikilinganishwa na
wagonjwa laki tano wanaogundulika na saratani ya shingo ya kizazi.


"Takwimu duniani kote saratani ya matiti ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 kila mwaka wanagundulika ikilinganishwa na wagonjwa laki 5 wanaogundulika na saratani ya shingo ya kizazi," alisema Mwaiselage

"lakini ieleweke kuwa saratani ya mlangi wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuwa na asilimia 35-40 ya wagonjwa wote huku saratani ya matiti ni asilimia 10-15," aliongeza.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Wauguzi kutoka hospitali ya Agha khan,k Lucy kway alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikiungana na taasisi ya ocean road katika kutokomeza magonjwa ya saratani.

"Kwa kufanikisha kutolewa kwa elimu juu ya saratani na upimaji wa bure wa ugonjwa huo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tunatoa elimu kupitia madaktari bingwa kutoka katika hospitali yetu hivyo wadau mbalimbali wajitokeze kushiriki na kuchangia katika kampeni ya kutokomeza saratani," alisema dk kway.










Pamoja na hayo Dr Mwaiselage ,amesema kuwa  taasisi ya saratani ya ocean road kwa kushirikiana na hoteli ya Kunduchi beach na Hospitali ya Agha Khan imeandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika kesho Oktoba 28 2017 na kuhudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu.

Kila mwaka mwezi oktoba umetegwa na jumuiya ya kimataifa kuhamasisha uelewa kwa jamii kuhusu juu ya saratani ya matiti pamoja na kuongeza uelewa.


Hivyo wananchi huhamasishwa kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na  ugonjwa huo.



Katika mwaka 2016/2017, taasisi ya ocean road ni taasisi ya pekee ya umma iliyobeba kwenye matibabu ya saratani ambapo ilihudumia wagonjwa 27,907 huku wagonjwa wapya wakiwa 6,338 na wale wa marudio wakiwa 21,569.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here