Afisa Msaidizi wa Forodha wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambazo ni
magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake
Mshtakiwa amesomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana
makosa mawili.
Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika
maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa
Msaidizi wa Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake,
kinyume na sheria.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akimiliki magari 19 ambayo
ni Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum,
Toyota Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex,
Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso, Suzuki
Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.
Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30,
2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha
juu yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.
Wakili Peter amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika,
hivyo anaomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya
awali (PH).
Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia Wakili Elisalia Mosha
aliiomba Mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo
yanadhaminiika kisheria.
Hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja
atakayesaini bondi ya Tsh. Milioni 20 ambapo alikidhi masharti na kuachiwa huru
kwa dhamana. kesi imeahirishwa hadi Novemba 7, 2017.

No comments:
Post a Comment