WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI JIPYA DODOMA KAMPUNI YA ALAF. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, September 23, 2017

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI JIPYA DODOMA KAMPUNI YA ALAF.

WINGU LA HABARI
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF  Dodoma. Kushoto ni Meneja Mkuu Upauaji (roofing) wa Kampuni ya mabati  ALAF, Dipti Mohanty  akishuhudia ufunguzi huo.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha Mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148.

Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali  kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo  na  kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”.

Kufunguliwa kwa tawi hili  kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani kwani wateja kutoka Dodoma na Singida sasa wataweza kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF.

Tunauza bidhaa zilizo tayari kwa matumizi kulingana na mahitaji ya mteja hasa mabati ya rangi  pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi na kiutaalamu. Kwa sasa kiwanda chetu cha ALAF kina matawi manne Mbeya, Mwanza, Arusha na Dodoma.

Kuhusu kampuni ya ALAF
Kampuni ya ALAF ni sehemu ya kampuni ziliyoko chini ya Kampuni   ya SAFAL, kampuni inayoongoza bila mpinzani ktika utoaji wa bidhaa bora za uezekaji barani Afrika.Kampuni ya SAFAL inaendesha shughuli zake katika nchi 13 kuanzia mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

Tukiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika biashara, ALAF tunaongoza  katika uzalishaji  wa bidhaa za  uezekaji za chuma.Katika kuongezea bidhaa zake za upauaji, bidhaa za kitaalamu pia zinauzwa na ALAF kama misumari (fixtite fastener), steel pipes, na Hollow section pamoja na viambatanisho muhimu kwa uezekaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here