JESHI LA POLISI TANGA LAPIGA MARUFUKU VIGODORO - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, September 27, 2017

JESHI LA POLISI TANGA LAPIGA MARUFUKU VIGODORO

WINGU LA HABARI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu.

Akiongea ofisini kwake Kamanda Benedict amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro, ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya uhalifu.

“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu”, amesema R.P.C Benedict.

Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here