Ripoti mpya ya Umoja wa
Mataifa imesema ukiukwaji wa haki za watoto katika maeneo yaliyo na vita
umeongezeka mwaka uliyopita, hususan nchini Afghanistan, Syria, Yemen, Iraq,
Somalia pamoja na Sudan Kusini.
Ripoti hiyo ya kila mwaka
kuhusu watoto katika maeneo ya vita imesema tangu Umoja wa Mataifa ulipoanza
kuweka kumbukumbu ya vifo vya raia na majeruhi mwaka 2009, idadi kubwa
zaidi ya watoto waliojeruhiwa imerikodiwa nchini Afghanistan.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa maelfu
ya watoto ni miongoni mwa watu 250,000 waliouawa nchini Syria. Na nchini Yemen
idadi ya watoto wanaotumiwa katika vita na pande zinazopigana imeongezeka mara
tano mwaka jana ikilingamnishwa na mwaka juzi.
Aidha nchini Somalia
ukiukwaji wa haki za watoto umeongezeka kwa asilimia 50.
No comments:
Post a Comment