MKEMIA MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAINGIZAJI WA KEMIKALI - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, August 17, 2017

MKEMIA MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAINGIZAJI WA KEMIKALI


Mkemia mkuu wa serikali Profesa Samwel Manyere akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vigezo vya uingizaji Kemikali.
WINGU LA HABARI
Wafanyabiashara wanaongiza Kemikali nchini pasipo kufata utaratibu wapigwa marufuku kuigiza kemikali hizo hadi pale watakapofata sheria na kanuni zilizopo.
Mbali na kufata sheria zilizopo, wafanyabiashara hao wametakiwa kuingiza mizingo hiyo ikiwa na label yenye lugha ya Kiswahili au kiingereza kama ilivyoelekezwa kwenye jedwali la 19 katika kanuni za Sheria ya Usimamizi na Udhibiti.
Akizungumza na Waandishi wa Habari -, Profesa Samwel Manyele amesema kuwa sheria inamtaka anayeingiza kemikali nchini lazima aweze amesajiliwa.
Profesa Manyele amesema kuwa sehemu ya tatu ya sheria kwa kuzingatia kifungu cha 11-28 inamtaka mfanyabiashara awe amepewa hati ya usajili (Certificate of Registration) kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 29 kabla ya kuanza kujishughulisha na biashara.
Amefafanua kuwa sehemu ya pili ya kanuni za Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali ya mwaka 2015, kanuni ya 3(1) (e) inaelekeza kila mdau wa kemikali aliyesajiliwa na kupata hati ya usajili inapaswa kuomba kibali cha kuingiza kemikali nchini.
“Wafanyabiashara wengi wamekuwa na utaratibu wa kuagiza kwanza mizigo na inapowasili ndipo wanaaza kuomba kubali lakini ni kinyume cha sheria” amesema Profesa Manyele.
Hata hivyo amebainisha kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni pamoja na kuingiza mizigo kabla ya kuomba kibali na kusababisha mrundikano wa mzigo bandarini inayosubiri vibali na ukaguzi.
Amesema kuwa wadau wengi wamekuwa na uelewa mdogo wa kisheria na kanuni zake kutokana na kuwatumia Mawakala wa forodha (Agents) bila wao wenyewe kufika kwa ajili ya kuonana na watendaji wanaotoa vibali na ukaguzi.
Profesa Manyele amesema licha ya changamoto zilizopo lakini wanaendelea kuwaelimisha wadau kuhusiana na matakwa ya sheria na kanuni zake juu ya uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.
Mwisho.







    

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here