JUKATA KUDAI MAANDAMANO MAHAKAMANI - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, November 4, 2017

JUKATA KUDAI MAANDAMANO MAHAKAMANI

Mwenyekiti wa JUKATAHebron Mwakagenda katikati akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam
Jukwaa la Katiba Tanzania (JAKATA) imeaandaa jopo la Mawakili 10 kwa ajili ya kwenda mahakamani kupinga katazo la Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuhusu kutofanya maandamano ya amanai  yaliopaswa kufanyika Oktoba 30 mwaka huu.
Uamuzi huo umekuja baada ya kupokea barua ya katozo la kutofanya maandamano hayo kutoka jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam
.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa JUKATA, Hebron Mwakagenda amesema kuwa sehemu ya barua kutoka jeshi la polisi imebainisha sababu ya katazo hilo ikiwemo Mhe. Rais DK. John Pombe Magufuli hajadhibitisha kushuriki maandamano hayo.

Amesema kuwa miongoni mwa sababu nyengine maandamano hayo ni marefu ambapo yanaweza kuathiri shughuli na kufanya barabara pamoja na siku ya maandamano ilikuwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaaza mithiani.

“Kutokana na sababu za jeshi la polisi JUKATA tumeamua kufungue kesi mahakamani kudai haki ya ambayo inaminywa na jeshi la polisi kwa kutumia sababu nyepesi” amesema Mwakagenda.

Amefafanua kuwa JUKATA ipo kwenye hatua ya mwisho za kutekeleza maamuzi hayo kwa kutumia mawakili wasomi zaidi ya 10 wakiongozwa na Dkt. Regemeieza Nshala katika mchakato wa kudai haki ya kufanya maandamano ya amani.

Mwekagenda ameeleza kuwa wameamua kwenda mahakamani kutokana duniani kote katika nchi za kidemokrasia zinazofuata utawala wa sheria , Mhimili wa mahakama ndicho chombo mahususi cha kutoa haki pale watu wanapoona haki zao zimenyimwa  na zimekandamizwa.

“Kama tukikosa haki katika mahakama za ndani basi tutaenda mahakama za nje kuitafuta” amesema Mwekagenda.

Amesema sababnu nyengine ya kwenda mahakamani ni kuomba tafri ya mahakama kuihusu namna ya jeshi la polisi linavyotumia vifungu 43 (3) na 44 vya sheria ya jeshi la polisi ya mwaka 2002.

“Kwa mtazamo na uchambuzi wetu jeshi la polisi limekuwa likitumia vibaya vifungu hivyo kuzuia mikutano pamoja na maandamano ya amani kinyume na uhalisia wa vifungu hivyo kwa kusema kuwa kuwa kuna uvunjifu wa amani” amesema Mwekagenda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here